“Msiende kudhalilisha serikali,Tume ya Uchaguzi inewatuma kwenda kuboresha Dafari la kudumu la Wapiga Kura’’ ni maneno ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Ileje Ndg.Haji Mnasi wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kwa watakaohusika na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mnasi alisema hayo alipokuwa akifunga mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Mwala mjini Itumba Ileje ambapo zaidi ya watu 370 wamewezeshwa jinsi ya kuboresha daftari kwa njia ya BVR.
Aliongeza kuwa kazi hiyo ni ya serikali hivyo wateule hao hawana budi kubeba taswira ya serikali kwa kufanya yale waliyotumwa badala ya kuzalisha matukio mabaya yanayoweza kudhalilisha serikali kupitia zoezi hilo.
Msimamizi huyo alibainisha baadhi ya mambo hayo kuwa ni ushabiki kisiasa,mavazi yasiyofaa,lugha za matusi na vitisho kwa wapiga kura pamoja na kunywa pombe wakati wa kazi hiyo.
Hassan Mwandoba Mkurugenzi Msaidi kutoka Tume ya Uchaguzi kitengo cha Ufuatatiliaji na Tathimini aliwataka wanamafunzo kusimamisha mambo yao binafsi ili kuweza kukamilisha zoezi hilo muhimu kwa kuwa waliomba wenyewe ajira hizo za muda.
Akizungumza kwa niaba washiriki Mwenyekiti wa mafunzo hayo Ndg.Mwanyemele aliahidi kuzingatia sheria katika kazi hiyo na kuhakikisha Ileje inafanya vizuri.
Zoezi hilo la uboreshaji wa wapiga kura linatarajiwa kuanza tarehe 26, Oktoba na kumalizika Mosi,Novemba 2019 yakiwa maandalizi kwaajili ya Uchaguzi Mkuu hapo mwakani.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa