Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Farida Mgomi, leo Julai 15, 2025, amefanya ziara ya kukagua maandalizi ya maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Nanenane jijini Mbeya.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mgomi alipata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za maandalizi ya banda la Wilaya ya Ileje, huku akiwataka wataalamu kuhakikisha wanaandaa mabanda yenye ubunifu, elimu na ubora ili kuonesha mafanikio ya sekta ya kilimo na mifugo wilayani humo.
Aidha, alisisitiza ushirikiano wa pamoja baina ya wataalamu, wakulima na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha Ileje inaendelea kung'ara katika maonesho hayo muhimu kitaifa.