A : MAJUKUMU YA KITENGO CHA TEHAMA
B : Hali ya Mifumo ya TEHAMA
Wilaya ya Ileje ina mifumo ya TEHAMA kumi na mbili (12), inayowezesha utendaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za Serikali, Mifumo hii imesaidia kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali, kuhifadhi na kuchakata taarifa za kiutumishi, kupanga mipango na bajeti, na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma. Baadhi ya mifumo hiyo ni Mfumo wa Kuripoti kazini watumishi, Mfumo wa taarifa za afya na usimamizi wa Mapato (GOTHOMIS), Mfumo wa Utumishi na rasilimali watu (HCMIS), Mfumo wa uthibiti wa malipo (MUSE), Mfumo wa mapato (LGRCIS), Mfumo wa usajili wa wanafunzi kwa shule za msingi (PREM), Mfumo wa mpango wa bajeti (PLANREP), Mfumo wa kusimamia malipo kwa kaya masikini chini ya mpango wa TASAF (PSSN), Mfumo wa mikopo ya asilimia kumi (TPLMIS), Mfumo wa takwimu kwa shule za msingi (Sensa Elimu Msingi-BEMIS), Mfumo wa bima ya afya iliyoboreshwa (IMIS-CHF) na Mfumo wa Facillity Financial Accounting Reporting System (FFARS), Mifumo hii yote inafanya kazi na pindi inapotokea changamoto tunasaidiana na wataalam wa TEHAMA wa TAMISEMI kutatua changamoto zinazojitokeza.
Huduma za Mawasiliano ya simu na Mitandao
Hadi sasa Wilaya ya Ileje inapata na kutumia huduma ya mtandao (internet) na kupata mawasiliano ya simu kupitia mitandao ya simu ya TTCL, VODACOM, TIGO, AIRTEL na HALOTEL.
Tovuti za Halmashauri
Wilaya ya Ileje imefanikiwa kuanzisha tovuti ya wilaya inayopatikana kupitia tovuti ya Halmashauri ya Wilaya kwa jina la www.ilejedc.go.tz. Tovuti hii inaendeshwa na Halmashauri kwa ushirikiano wa kitaalam na mamlaka ya serikali mtandao (eGA). Tovuti hii inasaidia kurahisisha mawasiliano kati ya jamii na Halmashauri.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa