Shirika la Uhamiaji Duniani (IOM) limeendesha semina ya mafunzo kwa wataalamu wa afya kutoka Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, yenye lengo la kuimarisha uwezo wa ufuatiliaji wa magonjwa katika maeneo ya mipakani.
Mafunzo hayo yamefanyika mapema leo Septemba 25, 2025 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa uliopo Nselewa, Wilayani Mbozi, mkoani Songwe, yakihusisha wataalamu wa afya, viongozi wa mila pamoja na viongozi wa dini kutoka Ileje na Tunduma.
Mafunzo hayo yamelenga kuboresha uelewa wa washiriki juu ya namna bora ya kudhibiti na kufuatilia magonjwa yanayoweza kusambaa kwa haraka kutokana na mwingiliano wa watu katika maeneo ya mpaka wa Tunduma na Isongole yanayounganisha Tanzania na nchi jirani ya Zambia.
Kupitia mafunzo hayo, washiriki walijifunza matumizi ya ramani ya uhamiaji wa watu (population mobility mapping) ili kubaini maeneo hatarishi yanayoweza kuchochea kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na hivyo kurahisisha maandalizi ya mikakati ya kinga na majibu ya haraka.
Vilevile, kupitia semina hiyo washiriki walipata nafasi ya kufanya majadiliano pamoja na kupata mawazo mapya yatakayotumika katika kutatua na kuzuia magonjwa ya milipuko katika maeneo ya mipakani ya Wilaya ya Ileje na Halmashauri ya Mji wa Tunduma iliyopo Wilaya ya Momba.
Aidha, IOM imesisitiza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya wataalamu wa afya wa pande.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa