Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Jabir Omar Makame, ameongoza hafla ya kuwakaribisha Madaktari Bingwa wa Samia waliowasili mkoani humo kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi. Hafla ya kuwapokea madaktari hao imefanyika mapema leo Septemba 15, 2025 katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa zilizopo Nselewa, Wilayani Mbozi, mkoani Songwe.
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Makame amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo muhimu za afya, akibainisha kuwa madaktari hao watakuwa wakitoa huduma katika hospitali zote za wilaya zilizopo mkoani humo.
Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza jitihada za kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi kupitia mpango huu wa Madaktari Bingwa, ambao umekuwa mkombozi kwa Watanzania wengi hususan walioko vijijini.
Uwepo wa kambi maalumu ya matibabu bingwa kwa wananchi umekuwa agenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha ustawi wa wananchi kupitia afya unaimarika kwa kusogeza huduma za kibingwa pamoja na unafuu wa huduma.
Madaktari Bingwa waliowasili katika Mkoa wa Songwe ni pamoja na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Daktari Bingwa wa Watoto na Watoto Wachanga, Daktari Bingwa wa Upasuaji, Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno, Daktari Bingwa wa Usingizi na Ngazi, pamoja na Muuguzi Mbobezi. Aidha, timu hiyo ya wataalam wa afya inaanza kambi maalum ya matibabu ya kibingwa kwa wananchi wote wa Mkoa wa Songwe katika hospitali zote za wilaya kuanzia leo Septemba 15 hadi 19, 2025.
|
|
|
|
|
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
|
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa