Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeendesha semina maalum kwa wawakilishi wa vyama vya siasa wilayani Ileje, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Semina hiyo imelenga kutoa elimu kuhusu sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi pamoja na kuwakumbusha viongozi wa vyama umuhimu wa kuendesha siasa kwa amani, mshikamano na kuheshimiana. Aidha, washiriki wamekumbushwa wajibu wao katika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia demokrasia na misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika semina hiyo, mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bwana Frank Shija, amevitaka vyama vya siasa kufanya siasa kwa kutambua haki na wajibu wao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 huku akiwasisitiza kuzingatia kanuni na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC). Pia amesisitiza umuhimu wa kufanya siasa safi na kampeni zisizovunja amani na utulivu katika maeneo yao na nchi kwa ujumla.
Aidha, Bwana Shija amewataka wawakilishi wa vyama vya siasa kuepuka vitendo vya rushwa sambamba na kuwa daraja la ushirikiano katika kuhakikisha zoezi la uchaguzi linafanikiwa kwa kiwango kinachostahili.
![]() |
![]() |
![]() |
|
![]() |
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa