Ziara hiyo ya siku moja ilimwezesha kufika hadi kwenye daraja la Mto Songwe linalounganisha Tanzania na Malawi huku akipata fursa ya kukutana na viongozi wa Wilaya ya Chitipa- Malawi waliokuwa na ziara pia katika mpaka huo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na viongozi wa Wilaya ya Ileje,Chitipa - Malawi pamoja na wakazi wa Kijiji cha Isongole Mhe.Mbarawa amewataka wakazi wa pande hizo mbili kutumia vema fursa zinazotokana na uwepo wa barabara hiyo ya kisasa.
Aliongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo umetumia teknolojia ambayo imetumiwa sehemu tatu tu hapa nchini ambazo ni kule Makete pamoja na Tabora.
Amesema kuwa gharama hizo kubwa za ujenzi zinaonesha dhamira ya serikali katika kufungua milango a biashara mpakani,akitoa wito kwa wote katika kuitunza kwa kuepukana na vitendo vinavyoharibu barabara.
Pamoja na mambo mengine waziri huyo alitoa ufafanuzi wa kero,maswali na maoni yaliyotolewa na wananchi likiwemo la ufungaji wa taa katika barabara hiyo.
Viongozi wa Wilaya hiyo wameendelea kutoa pongezi kwa serikali kutokana na mradi huo mkubwa pamoja na miradi mingine katika sekta mbalimbali.
Mhe.Anna Gidarya amesema kuwa mapato ya halmashauri yamekuwa yakipanda siku hadi siku kutokana na barabara hiyo.
Tangu kukamilika kwa barabara hiyo fursa za kibiashara hususani ya chakula toka nchi za Malawi,Zambia na Msumbiji zimeongezeka.
Ziara za viongozi wa serikali katika maeneo mbalimbali hapa nchini hulenga katika kufuatilia namna Ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyotekelezwa katika kuwaletea wananchi maendeleo
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa