Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Ndg.Matias Haule alipokuwa akizungumza na watalaam wa Idara hiyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Afisa huyo ameitaja mikoa itakayopitiwa na zoezi hilo kuwa ni Songwe,Kigoma na Mbeya huku akizitaja Hamashauri za Wilaya ya Ileje,Mji Tunduma na Songwe kunufaika pia katika mkoa wa Songwe.
Akizungumzia marufuku ya mikesha kwa watoto chini ya miaka 18 iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe.Anna Gidarya hivi karibuni inayolenga kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya unyanyaswaji na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na sekondari Haule amesema.
Naye Rodrick Sengela Afisa Maendeleo ya Jamii Wilayani humo amevitaja vijiji vya Ilulu,Ikumbilo na Mtima kuwa vitahusika na majaribio hayo.
Wakizungumza wakati wa zoezi hilo baadhi ya wananchi walioshiriki kutoa maoni yao katika Kijiji cha Mtima Kata ya Mbebe wamesema kuwa kutengana kwa wanadoa kumekuwa kikwazo kikubwa katika malezi ya watoto.
Pendo Mwang’ambaamesema kuwa ndoa inapovunjika husababisha watoto kuyumba kimalezi na kuharibu mwelekeo wa maisha yao.
Ikumbukwe kuwa serikali,taasisi binafsi na wadau mbalimbali kwa pamoja wanachukua kila hatua katika kuwapigania watoto,hususani wa kike dhidi ya vitendo vinavyohatarisha usalama wao ukiwemo ubakwaji,mimba za utotoni ajira za watoto pamoja na kukatishwa masomo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa