Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi, amemtaka Mkandarasi anae husika na upanuzi wa Mtandao wa Bomba la maji kutoka Isongole Kwenda Ilulu kuzingatia Muda na Ubora ili kufanikisha mradi huo,utakaondoa zahama ya wananachi kukosa huduma ya maji Safi na salama katika Kijiji cha Ilulu.
Akizungumza mapema leo Machi 3, 2025 wakati wa Hafla ya utiaji Saini mkataba wa makubaliano ya utekelezwaji wa Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Bomba kutoka Isongole Kwenda Ilulu uliofanywa kati ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Bapi Groups Company Limited Jvnail It Construction Limited, DC Mgomi amewahmiza watekelezaji wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa muda ili wananchi wa Kijiji cha Ilulu wapate maji safi na salama .
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amemtaka Mkandarasi huyo kuzingatia thamani ya fedha ya utekelezwaji wa mradi huo utakaoleta tija kwa wananchi, katika hatua nyingine dc Mgomi ameahidi kumpa ushirikiano Mkandarasi ili kufanikisha kukamilika kwa mradi huo.
Mkataba wa Mradi wa upanuzi wa Mtandao wa Bomba kutoka Isongole kwenda Ilulu umegharimu kiasi cha shilingi 1,435,148,951.50/= ambapo utatekelezwa kwa kipindi cha muda wa miez 15 mara baada ya kusainiwa kwa mkataba. Aidha mradi huo unatarajia kunufaisha Wakazi wapatao 1653 waishio katika Kijiji cha ilulu kwa kupata huduma ya maji Safi na Salama.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa