Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ileje , limempongeza na kumshukurcu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa Fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo inayoleta Tija na Ahueni kwa Wananchi katika Wilaya hii.
Wakizungumza mapema leo February 13,2025 wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri wilayani hapa, Madiwani hao wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha ustawi wa Wananchi wa Wilaya hii kupitia Fedha mbalimbali za miradi ya maendeleo zinatolewa pamoja na usimamizi mzuri wa watendaji wa Serikali ili kuhakikisha Miradi hiyo inafanya kazi na kuleta tija kwa Wananchi.
Aidha wamempongeza Mkuu wa Wilaya hii Mheshimiwa Farida Mgomi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri B. Nuru Waziri Kindamba kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza vyema Miradi ya Serikali kwa kuzingatia Ufanisi, Ubora na Weledi ili kuhakikisha inaleta manufaa kwa wananchi wilayani hapa.
Katika Hatua nyingine , Baraza la Madiwani limemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuendelea kusimamia na kuhakikisha Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hii inakamilika kwa wakati, aidha wamewahimiza watumishi wa Halmshauri ya wilaya ya ileje kuendelea kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa kufanya kazi kwa bidi pamoja na kuzingatia nidhamu ya kazi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa