Afisa Mazingira wa Halmshauri ya Wilaya Ya Ileje,Frank Kisanga amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yetu katika kukabidhi vifaa vya ufugaji wa nyuki Pamoja vifaa vya ujenzi wa mabwawa ya Samaki katika vikundi mbalimbali vya maendeleo vilivyopo katika Kata za Malangali na kafule zilizopo wilayani hapa.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi million 34.7 vimekadhiwa mapema leo Novemba 11, 2024 katika Kata za Malangali, Kafule na kijiji cha Kapelekesi ambapo kuna vikundi mbalimbali vya maendeleo vinavyojihusisha na shughuli za ufugaji wa nyuki Pamoja ufugaji wa Samaki. Vifaa hivyo vimefadhiliwa na Joint Songwe River Basin Commission (JSRBC) ambapo lengo kubwa ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka Bonde la Mto Songwe wilayani hapa.
Aidha Kisanga ametoa rai kwa vikundi hivyo, kuvitunza na kutumia vifaa hivyo kwa matumizi lengwa ili kuweza kuzalisha mazao yatokanayo na Nyuki Pamoja na Samaki kwa kiwango cha juu. Sambamba na hayo ameahidi kuwaletea wataalam watakaotoa semina juu ya matumizi sahihi ya vifaa hivyo, ili kujenga uelewa kwa vikundi hivyo kuvitumia vifaa hivyo kwa ufanisi.
Vifaa vilivyokabidhiwa kwa vikundi hivyo ni Pamoja na Mavazi ya Kurina asali( Bee suit), vifaa vya kurina (Bee tools) Mifuko 90 ya saruji, Mchanga tripu 6, Tofali Elfu 6, Kokoto tripu 6 pamoja na Nondo za milimita 12 zikiwa 45.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa