Itumba-Ileje
Timu ya Soka ya Itumba Stars imendelea kuwa hatari kwa kuzichabanga timu zote inazokutanazo katika Tarafa ya Bulambya wilayani Ileje na kuendelea kutawazwa bingwa kila mashindano inayoshiriki.
Katika kuthibitisha hilo imeichapa timu ya Chavuma toka Ilulu Kata ya Isongole kwa magoli 3-2 katika fainali za kugombania ng'ombe.
Ushindi huu unamekuja zikiwa zimepita siku chache tangu ibebe mbuzi mnyama kwenye uwanja huo huo wa Mkude uliopo Itumba.
Ikumbukwe kuwa miaka kadha iliyopita timu hiyo iliwahi kung'ara katika mashindano mbalimbali na kuweza kuwakilisha mkoa wa Mbeya wakati ule katika ligi ya Taifa ngazi ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa