Na: Daniel Mwambene, Ileje
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe.Joseph Mkude alipokuwa akizungumza kwenye Mahafali ya Kwanza ya Kidato Cha Kwanza katika Shule ya Consolata
Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mh.Joseph Mkude amazitaka taasisi za elimu wilayani humo kuzalisha raia wema watakaokuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
Alitoa wito huo wakati wa Mahafali ya kwanza ya Kidato cha nne ya Shule ya Consolata Iliyopo kata ya Chitete ikimilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya.
Kiongozi huyo alizitaka shule kutozalisha raia watakaokuwa watumiaji wa madawa ya kulevya yanayoharibu tabia za vijana na kuwa mzigo kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Alisema shule ni mahali ambapo hutoa elimu dunia na elimu ya kiroho hivyo wahitimu wa taasisi hizo hawana budi kuwa vioo kwa tabia na mienendo yao katika kuunga juhudi za serikali kupambana na madawa ya kulevya.
Hata hivyo,mkuu wa Wilaya alifurahishwa na jinsi uongozi wa shule hiyo unavyotumia vema rasilimali zilizopo ikiwa ni pamoja na kuchimba visima vya maji,ufugaji wa kuku akiahidi kushirikiana nao katika zoezi la upandaji miti msimu wa mvua utakapoanza.
Kwa upande wao walimu na wanafunzi wa shule hiyo waliahidi kufanya vema kwenye Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
Akisoma risala yao kwa Mgeni Rasmi mwanafunzi wa kidato cha nne Jastini fungu alisema kuwa katika mitihani ya iliyopita ule wa kidato cha pili nay a utimilifu kwa mkoa wa Songwe walikuwa wakifanya vizuri ,hivyo wataibeba wilaya ya Ileje.
Hata hivyo shule hiyo imekuwa ikikabiriwa na matatizo kadhaa yanayopunguza kasi ya kufika malemgo yaliyokusudiwa likiwemo kukosa uzio imara,vifaa vya michezo na vyoo bora kwa walimu.
Shule ya Consolata ilianza ikiwa na wanafunzi 88 wakiwemo wa kike 48 na wa kiume40 kwasasa ina jumla ya wanafunzi 350.
Mambo yalivykuwa ukumbini, wahitimu wahitmu wa Kidato cha nne wakiburudisha kwenye mahafali ya
Kwanza Oktoba, 14, 2017.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa