George Kibona mwenyekiti wa chama hicho alibainisha kuwa mwaka 2016 zilikopeshwa jumla ya Shilingi 180,200, 000, mwaka 2017 milioni 177,810,000, 2018 zilikopeshwa milioni 176,140,000
Kibona ameongeza kuwa mwaka 2019 jumla ya shilingi milioni 162, 2400 000 zilikopeshwa huku tangu Januari hadi Juni mwaka huu zikikopeshwa milioni 29,533 519 huku zaidi ya wanachama 160 wakiendelea kunufaika na uwepo wa chama hicho.
Mwenyekiti huyo,ameongeza kuwa wamekuwa wakitoa huduma bora kwa wanachama kiasi cha kuweza kutunukiwa ngao ya uendeshaji bora wa SACCOS iliyotolewa 2018 na Tume ya Ushirika Tanzania akitoa wito wa watumishi wengine kujiunga na chama hicho.
Taarifa ya chama hicho imeeleza kuwa tangu kuanzishwa kwake mnamo 1994 zaidi ya shilingi Bilioni 1na Milioni 600 zimekopeshwa kwa wananchama wake na kuwawezesha kujenga nyumba za kuishi,kulipa ada za shule na kuanzisha shughuli za ujasiliamali.
Gaspalina Mwakabuta mmoja wa wanachama amesema kuwa amenufaika na SACCOS hiyo kwa kulipa ada za shule za watoto,kuboresha makazi na kuongeza mtaji kwenye ujasiliamali.
Mafanikio hayo yanakuja sanjali na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015 iliyolenga kuhakikisha kuwa shughuli zote zenye mwelekekeo wa ushirika zinapewa msukumo stahiki wa kuhamasisha na kusimamia kwa ngyuvu uanzishaji wa vikundi vya ushirika kama vile SACCOS na VICOBA
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa