Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela amepishana na DC na DED wa Ileje akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake wilayani Ileje.
Tukio hilo linakuja zikiwa zimepita siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli atie mguu mkoani humo akipongeza utendaji kazi wa viongozi wa mkoa huo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
RC Mwangela akifanya ziara ya kushitukiza alipishana na viongozi wa Wilaya hiyo ambao ni Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg.Joseph Mkude pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambao walikuwa wamekwenda vijijini kuhudumia wananchi.
Ziara yake hiyo ya kushitukiza iliyomfikisha katika Kata za Mlale,Isongole na Chitete ililenga kuangalia namna maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yalivyofikiwa ili kuwezesha uchaguzi huo kufanyika kwa usalalama.
Hilo likifanywa hivyo na Mkuu wa Mkoa,naye Mkuu wa Wilaya hiyo alikuwa yupo katika Kata ya Ibaba akishiriki kampeni ya kujisajili kwenye Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF),huku Mkurugenzi Mtendaji akiwa Kata ya Ngulugulu na wataalam wa Idara ya ardhi kupima eneo la kujenga Kituo cha Afya na baadaye aliungana na DC kwenye mkutano na wananachi wa Ibaba.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Ibaba Mkuu wa Wilaya alisema kuwa licha ya kuwa na ugeni wa Mkuu wa Mkoa wilayani kwake aliruhusiwa aendelee na ratiba zake ili kuwaepushia wananchi usumbufu kwakuwa walikuwa wamejiandaa kukutana na kiongozi wao.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa