Ileje-Songwe
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya kupokea wanafunzi hao katika Sekondari ya Itumba Mkude amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wanafunzi wengi huchelewa kusajiliwa na kuanza masomo ya Kidato cha Kwanza pamoja na Darasa la Kwanza katika Wilaya yake kwasababu ya kukosa sare za shule.
Ameongeza kuwa si sare tu zimeonekana kuwa kikwazo bali hata michango mingine ikiwemo ile ya chakula ambayo amesema isiwe chanzo cha kutowasajili watoto hao .
“Watoto wasizuiliwe kusajiliwa kwasababu ya kutokuwa na sare,wasajiliwe kwanza huku wazazi na walezi wakiendelea kuwakamilishia mahitaji yao mengine hii inatusaidia kupata taarifa sahihi za wanafunzi”.
Amesema,kutowasajili wanafunzi mapema hukwamisha upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa wakati kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo,Mkude amekiri kuwa kutokuwa na sare kutaweza kupunguza mwonekano wa uanafunzi lakini utasaidia kupata takwimu sahihi mapema.
Akizumgumzia maandalizi ya mapokezi ya Kidato cha Kwanza mwaka huu 2021 Ndg.Haji Mnasi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema kuwa maandalizi yanakwenda vema wanatumia muda mrefu katika maeneo ya kazi ili upungufu wa vyumba tisa vya madarasa ukamilishwe kabla ya masomo kuanza.
Jumla ya wanafunzi 1800 wanatarajiwa kuanza kidato cha Kwanza kwenye shule 24 za serikali na 3326 Darasa la Kwanza kwenye Shule zote 83 za Msingi wilayani humo
Hadi sasa Wialaya ya Ileje ina jumla ya Shule za Sekondari 22 zikiwemo za serikali 19 na 3 za
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa