Katika kuadhimisha Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Farida Mgomi, leo ameongoza wakazi wa Kata ya Isongole katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kuenzi Muungano huo muhimu kwa historia ya Tanzania.
Zoezi hilo limehudhuriwa na wakazi wa maeneo mbalimbali, viongozi wa serikali za mitaa, pamoja na watumishi wa umma, ambapo walishiriki kusafisha maeneo ya masoko, barabara na maeneo ya taasisi za umma.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mheshimiwa Farida Mgomi amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kuonesha mshikamano katika kusherehekea Muungano kwa vitendo. Aidha, ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwaasa wananchi wote wa Ileje na Tanzania kwa ujumla, kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mheshimiwa Mgomi pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha amani, Umoja na Mshikamanano miongoni mwa Wananchi, akibainisha kuwa haya ndiyo Misingi iliyojenga Taifa lenye umoja na uthabiti kwa kipindi cha zaidi ya nusu karne.
Maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano mwaka huu yamebeba kaulimbiu ya kuhimiza mshikamano wa Kitaifa, Uzalendo na Ushiriki wa Wananchi katika maendeleo ya Taifa. Ambapo kauli mbiu ilisema “Muungano wetu Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa Shiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa