Mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo yameandaliwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kwa kushirikiana na PS3+ ambao ni Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Serikali kwa ufadhili wa (USAID)
Akizungumza kwenye mafunzo Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo Ndg.Gilbert Mbowe alisema kuwa kupitia mafunzo hayo Wahe. Madiwani watajifunza sheria mbalimbali zinazowahusu,kuzijua kanuni na taratibu za usimamiaji na uendeshaji vikao,nidhamu na uongozi.
Mtalaam huyo aliongeza kuwa MUKI ambao ni Mfumo wa Ujifunzaji kwa njia ya Kielekroniki (yaani Elimu Masafa) utawasaidia wahe.madiwani kujifunza wakati wowote na mahali popote.
Pamoja na mambo mengine madiwani watakapokuwa wamesoma na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mfumo huu watakuwa na uwezo wa kujibu maswali na kutunukiwa vyeti kutoka chuo hicho cha Serikali za Mitaa Hombolo.
Mhe.Ubatizo Songa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amewashukuru watalaam wa Halmashauri kwa kufanikisha zoezi hilo ambalo lilikuwa ombi lao la muda mrefu mara baada ya kuchaguliwa mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumzia teknolojia ya kidijitali Mhe.Songa alisema kuwa,njia hiyo itapunguza gharama ambapo Wahe.Madiwani wangeweza kusafiri hadi chuoni Dodoma badala yake watasoma wakiwa huko Ileje.
Kutokana na kukua kwa matumizi ya teknolojia kutoka anolojia na kwenda dijitali hii ni hatua nyingine kwa Wahe.Madiwani wa halmashauri hiyo ambao walishaachana na matumizi ya makablasha ya makaratasi wakitwa wanatumia vishikwambi.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa