• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Matangazo |
Ileje District Council
Ileje District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Core Values
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Mipango, Tathimini na Takwimu
      • Elimu Sekondari
      • TASAF
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Fedha
      • Utamaduni na Michezo
      • Mawasiliano ya Serikali
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa mazingira
    • Kata
      • Isongole
      • Itumba
      • Bupigu
      • Mbebe
      • Chitete
      • Malangali
      • Ikinga
      • Kafule
      • Kalembo
      • Lubanda
      • Luswisi
      • Ibaba
      • Itale
      • Ndola
      • Ngulilo
      • Mlale
      • Ngulugulu
      • Sange
    • Taasisi za Serikali
    • Mashirika ya Umma
    • Ofisi ya Mkuu Wa Wilaya
    • Ofisi ya Mbunge
    • Vyama vya Siasa
    • Viongozi wa Dini na Mila
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vituo vya Utaliii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Fedha
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha
    • Ratiba ya Vikao
    • Kuonana na Mh. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyothibitishwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari za mkoa
    • Habari za kitaifa
    • Habari za kimataifa

KAMATI YA FUM YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI ILEJE

Imewekwa: May 19th, 2025

Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango (FUM) ya Halmashauri ya Wilaya ya Ileje imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo. Ziara hiyo ililenga kutathmini hatua za utekelezaji wa miradi yenye lengo la kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi, hususan katika sekta za afya, elimu, mazingira na utawala.

Katika tarafa ya Bulambya, kamati hiyo ilikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya wilaya – Itumba, ambapo halmashauri imepokea shilingi milioni 350 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ambao umefikia asilimia 80 ya utekelezaji. Pia walikagua jengo la utawala la halmashauri ambalo limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2, pamoja na mradi mkubwa wa upanuzi wa shule ya sekondari Izuba kwa ajili ya kuanzisha kidato cha tano na sita, ambao unajumuisha madarasa manne, nyumba moja ya watumishi (2-in-1), mabweni mawili, na vyoo, kwa gharama ya shilingi milioni 480.

Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari ya wasichana Ileje unaogharimu shilingi milioni 130 na ambao umefikia asilimia 30 ya utekelezaji, pamoja na mradi wa usafi na mazingira katika zahanati ya Ikumbilo unaohusisha ujenzi wa kichomea taka, mashimo ya majivu na kondo la nyuma kwa akina mama waliojifungua, pamoja na sehemu ya kunawia mikono, kwa gharama ya shilingi milioni 16.5.

Kamati ya FUM imetoa pongezi kwa wasimamizi wa miradi hiyo kwa usimamizi thabiti na utekelezaji mzuri wa miradi, huku ikisisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili ianze kutoa huduma stahiki kwa wananchi. Vilevile, kamati hiyo imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia wilaya hiyo fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hatua inayochochea ustawi na maendeleo ya wananchi wa Ileje.

Matangazo

  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA TAREHE 1 MEI HADI 7 MEI 2025 April 28, 2025
  • TANGAZO LA KUFANYA USAFI SIKU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR April 25, 2025
  • Tembelea Zote

Mpya

  • KAMATI YA FUM YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI ILEJE

    May 19, 2025
  • Katika tarafa ya Bulambya, kamati hiyo ilikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya wilaya – Itumba, ambapo halmashauri imepokea shilingi milioni 350 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ambao umefikia asilimia 80 ya ut

    May 19, 2025
  • Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Songwe

    May 01, 2025
  • Bi. Kindamba: Weledi na Uaminifu ni Nguzo Kuu Katika Uandikishaji

    April 29, 2025
  • Tembelea Zote

Video

DD
Video Zaidi

Tovuti Mashuhuri

  • UTUMISHI WA UMMA
  • OR - TAMISEMI
  • Songwe Region
  • ILEJE DISTRICT COUNCIL FACEBOOK
  • TAUSI PORTAL

Kurasa za Karibu

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa