Na Daniel Mwambene,Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Hili ni moja ya mabwawa mawili yanayomilikiwa na Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Ileje Ndugu Gidioni Kibona yakiwa nyumbani kwake mjini Itumba.
Halmashauri ya Wialaya ya Ileje mkoani Songwe ina zaidi ya mabwawa 300 ya samaki yakimilikiwa na watu binafsi,taasisi na serikali.
Taarifa kutoka kwa Afisa Uvuvi wa Wilaya hiyo Ndugu Gidion Kibona na uchunguzi wa mwandishi wa habari hizi umebaini juu ya kuwepo kwa mabwawa mengi katika Kata za Lubanda,Sange na Itumba.
Mtaalam huyo wa samaki alisema kuwa kutokana na maendeleo katika sekta hii ya uvuvi tayari watu binafsi katika vijiji vya Itumba na Isongole wameanza kufuga samaki majumbani mwao wakitumia mabwawa rahisi.
Akielezea utalaam huo ,nyumbani kwake wakati mwandishi wa habari hizi alipotembelea mradi huo Ndugu Gidioni Kibona alisema kuwa kila mwananchi anaweza kuwa na bwawa rahisi nyumbani kwake ilmradi kuwe na upatikanaji wa maji kwa uarahisi.
Kibona anayemiliki mabwawa mawili nyumbani kwake amewataka wananchi kushirikiana na wataalam hao katika kuiendeleza sekta hiyo ikiwa ni hatua mojawapo ya kuondokana na umaskini.
Mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Sange ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa bwawa lao la shule limekuwa mkombozi kwao kila wanapopata ugeni kwani limekuwa likiwapatia kitoweo.
Uchunguzi pia umebaini juu ya kuwepo kwa mabwawa mengi zaidi katika Tarafa ya Bundali kuliko Tarafa ya Bundali kutokana na wingi wa maji kataka ukanda huo wa juu ambao hupata mvua kwa wingi.
Moja ya mabwawa matatu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ileje yaliyopo mjini Itumba.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa