Hayo yameelezwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo ukiwa ni mfululizo wa vikao hivyo kwa mujibu wa uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
Kutokana na mafanikio hayo pongezi zimeendelea kutolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiemo viongozi wa kisiasa.
Arbert Sitma Katibu wa Chama cha Mapinduzi (C.C.M) alisema kuwa umoja na ushirikiano kati ya Wahe.Madiwani pamoja na watendaji wa serikali ni miongoni mwa mambo yaliyosaidia kuleta matokeo hiyo.
Katibu huyo akashauri mapato hayo hayana budi kuendelea kuwanufaisha wananchi wote kulingana na maeneo yao badala ya kuwanufaisha wachache hali inayoweza kuvunja moyo wangine katika utendaji wa kila siku.
Matias Mizengo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo aliyezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg.Joseph Mkude alisema kuwa wao wakiwa wasimasimizi wa serikali za Mitaa wanaridhishwa na juhudi za Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo katika kukusanya na kudhibiti mianya ya ukwepaji ulipaji kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
Kupatikana kwa Hati Safi kwa miaka mitano mfululizo kumekuja Halmashauri hiyo ikiwa chini wa Mwenyekiti Mhe.Ubatizo Songa (Diwani wa Kata ya Bupigu) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Haji Mnasi hali inayothibitisha umoja,mshikamano na uwezo wa kutatua changamoto ndani ya Halmashauri hiyo.
Awali Mhe.Songa aliwaagiza watendaji wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha wanaendelea kutoa motisha kwa wakati kwa Watendaji wa Vijiji na Kata wanaofanya vema katika ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato.
Haji Mnasi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,alikieleza kikao kuwa wameweza kufikia asilimia 93.9% hizo kutokana na mikakati mathubuti waliyojiwekea ikiwemo kuwachukulia hatua watenda wazembe,kufanya doria mara kwa mara ili kubaini wakwepaji wa kulipa ushuru pamoja na ushirikiano mzuri uliopo na Ofisi ya DC.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa