Mhe.Mwampashi amechukua nafasi hiyo,iliyokuwa ikishikiliwa na Mhe.Noah Mwasile Diwani wa Kata ya Ngulilo (CCM)aliyemaliza muda wake akiwa alichaguliwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Katika uchaguzi huo,kura zilizopigwa zilikuwa za “Ndiyo’’ au “Hapana’’kutokana na kutokuwa na wagombea toka vyama vingine vya siasa,hivyo akaibuka kuwa mshindi akizoa kura zote za ndiyo kwa wajumbe waliohusika.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kiongozi huyo amaeahidi kuwa kiungo baina ya wahe.madiwani,watalaam,Serikali Kuu ,Chama cha Mapinduzi na wananchi wote kwa ujumla.
Kikao hicho cha Robo ya Nne kimefanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo kikijadili mambo kadhaa yakiwemo ya mapato pamoja na miradi ya maendeleo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa