Mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa Kamati ya Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg. Joseph Mkude alisema kuwa mafunzo hayo yamekuja kwa wakati mwafaka kwani bado vitendo vya ukatili vimekuwa vikiripotiwa katika jamii.
Mkude aliongeza kuwa licha ya kuwepo kwa vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto pia baadhi ya wanaume hunyanyaswa na wake zao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Ndg.Haji Mnasi alisema kuwa wajumbe hao wanatarajiwa kupeleka elimu kwa jamii ili kuendeleza kupunguza ukatilii na kuyawezesha makundi hayo kuishi kwa amani
Afisa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa aliyekuwa mwezeshaji alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kupunguza vitendo vya ukatili kutoka ngazi ya familia hadi taifa. Baadhi ya wajumbe waliomba serikali iongeze wigo wa kupokea matukio hata kwa wanaume kutokana na wanaume wengi kuona aibu kuripoti kwenye mamlaka husika juu ya ukatili wanaofanyiwa katika ndoa
Walisema kuwa wanaume wengi hukaa kimya wanapofanyiwa ukatili na wake zao kwa lengo kulinda hadhi za uanaume.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefadhiliwa na Shirika la UNICEF yanalenga kuwafanya wanawake na watoto ambao ni wahanga wakuu wa ukatili katika jamii kuwa katika hali ya usalama.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa