“Michango ya wananchi kwenye miradi ya ujenzi si pesa tu,pokeeni hata vitu vingine zikiwemo hata nguvu zao zithamanisheni”RC wa Songwe Mhe.Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela.
Alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya siku moja ya kufungua shule za msingi na sekondari baada ya mapumnziko ya mwezi mmoja akiangalia mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2020.
Katika ziara hiyo aliweza kutoa mifuko 80 ya saruji kwa shule nne za sekondari alizotembea ambazo ni Mbebe,Kakoma,Nakalulu na Itumba kila moja ikitarajia kupokea mifuko 20.
Akizungumza na katik Kata ya Mbebe RC Mwangela alisema kuwa kumekuwa na dhana potofu kwa baadhi ya viongozi na wananchi kuwa michango inayochangwa na wananchi baada ya kukubalina ni pesa tu hali aliyoipinga akisema ni upotoshaji.
Alisema kuwa,mwananchi anaweza kuchangia nguvu zake au vifaa vya ujenzi kama vile mbao na matofali na vitu hivyo havina budi kuthamanishwa ili kupata gharama za mradi.
Akizungumzia suala la kukamilisha majengo alisema viongozi hawana budi kukaa pamoja kwenye serikali za vijiji na kata katika kapanga mikakati ya ujenzi wa shule badala ya kusubiri kwanza matukio ya watoto kufaulu.
Kiongozi huyo aliweza kufurahishwa na uongozi wa Kata ya Isongole kwa jinsi wanavyoshirikiana na kuiweka wazi mipango yaujenzi wa shule huku akiutaka uongozi wa Kata ya Itumba na mambo yanavunja umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi.
Kwa upande wao walimu walimweleza kiongozi huyo kuwa walishajipanga kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ikiwemo kutumia vyumba vya akiba vilivyokuwepo pamoja na vyumba vya maabara kwa muda.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa