Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya Mhe.Farida Mgomi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo.
Akizungumza na wananchi kupitia Ileje Fm 105.3 kwenye kipindi maalum kufuatia vifo vya watoto wawili wa Darasa la Kwanza wenye umri wa miaka sita kila mmoja waliopoteza maisha wakizidiwa na maji ya Mto Kambekeswa walipokuwa wakiogelea.
Mhe.Mgomi alisema kuwa watoto wakiwa katika michezo yao ya kitoto wanakabiriwa na hatari nyingi ambazo mzazi au mlezi mmoja mmoja hawezi kuziona,hivyo zinahitaji jamii nzima kuchukua hatua kuhusu mazingira hayo hatarishi.
Kufuatia matukio hayo,aliwataka wananchi wote na viongozi wa ngazi mbalimbali kushikamana kufunika visima vyote vilivyopo katika maeneo yao,huku viongozi wa kata,vijiji na vitongoji wakiagizwa kusimamia zoezi hilo.
Jicho la kamera hii lilipopita kwenye anga za kijiji cha Isongole walipozikwa watoto hao ilinasa moja ya kisima kilichojaa maji na kudhihirisha kauli ya Mkuu wa Wilaya kuhusu uwepo wa visima visivyofunikwa.
Mara nyingi kila msimu wa mvua unapoanza kumekuwa kukitokea matukio mbalimbali ya watoto kufa maji kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumbukia kwenye visima visivyofunikwa.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa