Ileje Songwe
Pongezi hizo zimetolewa na Ndg.Haji Mnasi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo usiku wa kuamkia leo Ijumaa 18/2/2021 wakati wa kufanya doria ya kufuatilia wanaojaribu kukwepa kulipa ushuru wanapokuwa wakisafirisha bidhaa mbalimbali zikiwemo mbao na mazao.
Akizungumza na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo SPS Abdi Mchome katika Kitongoji cha Penzu kilichopo Isongole ambapo gari la mizigo aina ya Fuso lilibainika kuwa na mbao zilizozidi idadi zikilinganishwa na idadi iliyoandikwa kwenye stakabadhi Mnasi amesema kuwa msaada wa polisi waliokuwa doria chini ya OCD umewezesha kukamatwa kwa gari hilo.
Mnasi ameongeza kuwa halmashauri hiyo inahitaji sana wawekezaji na wafanyabiashara ili kuongeza mapato ya Halmashauri lakini haitawavumilia wafanyabishara wadanganyifu.
Akizungumzia kuhusu matukio hayo OCD wa Wilaya hiyo amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanajali na kuzingatia sheria za barabarani ili kuwalinda wao wenyewe na watumiaji wengine wa barabara.
Amesema kuwa licha ya jeshi hilo kusaidia katika kukusanya mapato bado watahakikisha kuwa vyombo hivyo vinakuwa salama ili kulinda usalama wa abiria na mali zao
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa