Katika kuhakikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo unakwenda vema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Ndugu Haji Mnasi ametembelea baadhi ya miradi hiyo na kupongeza hatua zilizofikiwa.
Miradi aliyotembelea ni pamoja na ukarabati wa vyoo vya standi ya Itumba ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya,ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Ndola,pamoja kushudia ubomoaji wa baadhi vyumba vya madarasa ili kupisha ujenzi mpya katika Shule ya Msingi Itale.
Akiwa katika stendi ya Itumba kiongozi huyo alimwagiza Afisa Mtendaji wa Kata hiyo kuhakikisha anakamilisha ukarabati huo ili kuwaondolea kero wananchi na kuepusha uwezekano wa kutokea kwa milipuko ya magonjwa .
Akiwa katika kata ya Itale ameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bi Mary Konga kuwa mapema leo tangu saa 12.00 zaidi ya wakazi 100 wa kijiji cha Itale wamefika shuleni hapo na kushirika ubomoaji wa vyumba viwili vya madarasa ili kupisha ujenzi mpya.
Pia akiwa kwenye shule shikizi ya Igwilizya iliyo chini ya Shule ya Msingi Itale pia alifurahishwa kwa kasi ya ujenzi pamoja na ubora wa majengo.
Viongozi wa kijiji hicho wamepongeza serikali kwa jinsi inavyotoa pesa kwaajili ya miundombinu ya shule hali waliyoielezea kuwa itachangia kuinia kiwango cha elimu huku wakiomba serikali iendelee kutoa ajira kwa walimu ili kuziba mapengo yaliyiachwa na wastaafu wengi.
Pia ziara hiyo ilimwezesha kufika hadi kwenye Shule Binafisi ya Shangwale iliyopo katika Kijiji cha Iwala na kukutana na uongozi wa shule hiyo kasha akawapongeza kwa jinsi wanavyoshiriki katika kuwaendeleza kielimu watoto wa Ileje na Watanzania kwa ujumla.
Mkuu wa shule hiyo Mwl.Clement Jewe alimweleza Mkurugenzi huyo kuwa licha ya shule hiyo kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali bado haijafikiwa na umeme wa gridi ya taifa.
Hadi sasa wilaya ya Ileje ina jumla ya shule za sekondari 22 zikiwemo za binafisi tatu ambazo ni Consolata,Mbagatuzinde pamoja hii ya Shangwale ilioanzishwa miaka ya hivi karibuni.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa