Wafanyabishara wanaotumia mpaka wa Ileje mkoani Songwe kuingia na kutoka hapa nchini wametakiwa kuzingatia kanuni na taratibu ili kuepuka usumbufu wanaoweza kuwapata pindi watakapobainika kukiuka sheria.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya haiyo wakati wa zoezi la kubaini uhalali wa tumbaku iliyokuaikisafirishwa kwenda nchi jirani.
Mkude alisema kuwa kila mfanyabiashara hana budi kuhakikisha kuwa anakuwa na nyaraka zote zinazomruhusu kusafirisha mizigo kuingia na kutoka hapa nchini.
Alisema kuwa zaidi ya tani tisa za tumbaku iliyokuwa ikitarajiwa kusafirishwa kwenda nchi jirani iliweza kubainika ikiwa imehifadhiwa kwenye nyumba ya mkazi wa Isongole huku mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa mmiliki wa mzigo akishikiliwa kwa muda fulani.
Mmoja wa wabebaji miigo (kuli) wa mizigo kijijini hapo alisema kuwa biashara ya kusafirisha tumbaku kwenda nchi za jirani imekuwa ikipamba moto siku hadi siku kutokana na kuonekana uwepo soko la zao hilo.
Mpaka wa Isongole-Ileje umekuwa ukipataumaarufu siku hadi siku ukiikimbilia mipaka ya Tunduma na ule wa Kasumulu-Kyela mkoani Mbeya.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa