Kikao hicho cha siku moja kimefanyika katika Ukumbi wa Sekondari ya Itumba kimeweza kuwakutanisha Kamati ya Usalama,Wah.Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo,Watendaji wa Vijiji na Kata pamoja na Wenyeviti wa Vijiji.
Yaliyojiri katika kikao hicho:
Maafisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya waliweza kutolea maelezo na majibu juu ya kero zilizokuwa zimetolewa hawa ni pamoja na Afisa Utawala na Utumishi,Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika,Mweka Hazina pamoja na Afisa Mifugo na Uvuvi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Geofrey Nauye pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Ubatizo walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa yaliyokuwa yameulizwa.
Pia Wahe.Madiwani waliweza kutoa maelezo juu ya kero zilizokuwa zimewasilishwa zikilenga maeneo yao.
“Kikao hiki ni muhimu kwetu kwani sisi ni watekelezaji na wasimamizi wa mipango ya serikali na wananchi ni mabosi wetu,tupo hapa wote ili tutoke na uelewa wa aina moja ili tuweze kuwahudumia vizuri hawa wananchi ambao huweka serikali madarakani”DC wa Ileje Mhe.Anna Gidarya.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa