Akizungumza katika ofisi yake hiyo mpya na viongozi wa wilaya waliofika kumpokea Mhe.Mgomi amesema kuwa anapenda sana mfumo wa utendaji kazi unaowafikia wananchi ili kuweza kubaini changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Ameongeza kuwa nafasi yake inampa mamlaka ya kusimamia shughuli zote za kiserikali ili wakazi wa Ileje waweze kuona matokeo chanya ya mipango ya serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na mambo mengine ametoa mwelekeo kuwa anapenda pia kufanya kazi kitimu,kiweledi na kudiriki badala ya kukata tamaa kwa kutafuta visingizio.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mhe.Rais Samia aliteua na kuhamisha baadhi ya wakuu wa wilaya ambao wanaendelea kula viapo na kuripoti katika vituo vyao vya kazi ili kuendelea kuwatumikia watanzania.
Katiaka mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe.Anna Jolam Gidarya amehamishiwa katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu..
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa