Jinsi ya Kufika Wilayani Ileje Mkoani Songwe
Ukitaka kufika wilayani Ileje kuna njia kadhaa unazoweza kuzitumia;
1.Mpemba-Isongole-Itumba (Makao Makuu ya Wilaya)
Mpemba ni kituo kilichopo njiapanda ya kwenda Ileje katika barabara kuu ya Mbeya-Tunduma.
Hii ni maarufu kuliko barabara zote za wilaya hii kwani huunganisha na wilaya ya Kyela kwa kupitia Isongole-Ndembo-Kyela.
Hii pia hutumiwa sana na watu wanaokwenda Malawi kupitia mpaka wa Isongole,ikitumiwa sana na wafanyabiashara wa nafaka hususani mahindi toka soko la kimataifa la Isongole chini ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula(NFRA).
Hupitika mwaka mzima ila wakati wa masika kuna baadhi ya maeneo ni sumbufu.
Hatua za awali za ujenzi kwa kiwango cha lami zilishaanza na kambi lipo katika kijiji cha Ikumbilo Kata ya Chitete.
2.Vwawa-Ilembo-Hezya-Mlale-Itumba.
Njia hii ni ya mkato kwa wanaosafiri kati ya Vwawa(Makao Makuu ya Mkoa wa Songwe) kwenda Itumba(Makao Makuu ya Wilaya ya Ileje)
Ni kiungo muhimu kati ya Wilaya ya Ileje mkoa na Wilaya ya Mbozi ikitumiwa zaidi kwa shughuli za kikazi.
Imejengwa kwa kiwango cha changarawe ikipitika mwaka mzima
3.Njiapanda ya Iyula-Kijiji cha Iyula-Mlale-Itumba:
Hutumiwana wasafiri wa kwenda Mbeya ikiunaganishwa na barabara kuu ya Mbeya –Tunduma.
Ni nzuri zaidi kuitumia wakati wa kiangazi kwani wakati wa masika kuna maeneo korofi katika Wilaya ya Mbozi.
4.Mbalizi-Ilembo (Mbeya Vijijini)-Iwiji-Itumba(Makao Makuu ya Wilaya).
Barabara hii hutumiwa na wanaokuja Ileje wakielekea Kata za Ngulilo,Itale,Ibaba na Ndola.
Ni maarufu sana kwa kusafirisha mazao ya mbao,abiria na bidhaa.
Wakati wa masika kile kipande cha Isangati(Mapengo) Mbeya Vijijini hadi Ngulilo(Ileje) na kile cha Shigamba(Mbeya Vijijini) hadi Ibaba(Ileje)zimekuwa hazipitiki vema hasa kwa magari ya mizigo.
5.Njia ya KKK-Ikuti(wilaya ya Rungwe)-Luswisi-Lubanda-Sange-Katengele-Ibungu-Isongole-Itumba(Makao Makuu ya Wilaya).
Hutumiwa na wasafiri wanakuja Ileje kwenda kata za Luswisi,Lubanda,Sange Ngulugulu,Kafule na Kalembo.
Kwa mtu anayetokea Mbeya akiwa hana shida Makao Makuu ya wilaya hana budi kutumia njia hii.
Ni moja ya njia zenye milima na miteremko mikali ikiwa ikileta shida wakati wa masika kwa baadhi ya maeneo.
Pia hutumiwa na wafanyabiashara wengi wa mbao toka maeneo hayo.
6.Kasumulu (Kyela)-Ndembo-Isongole-Itumba(Makao Makuu ya Wialaya)
Ni kiunganishi kikubwa kati ya Ileje ne Kyela hasa kwa wafanyabiashara wakiwemo wale wa nyungo toka kata za Ikinga,Kafule na Malangali.
7.Mbilima-Chitipa (Malawi) hadi Isongole-Ileje(Tanzania)
Hii njia ni mlango wa kuingia na kutokea Tanzania na Malawi.
Ni moja ya barabara zenye kutoa matarajio makubwa kwa wilaya hii mara zitakapounganishwa kiwango cha lami huku Tanzania kazi za awali zikiwa zimeanza.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa