Zoezi hilo la siku tatu lilianza hapo Jumatatu linatarajiwa kukamilika hapo Jumatano linatarajiwa kuvifikia vijiji 50 katika Wilaya ya Ileje linahusu uhakiki wa kundi hilo kwa njia ya kielekroniki (yaani mfumo) likiwa limetanguliwa na mafunzo ya siku mbili kwa wataalam wa Halmashauri kutoka.
Akizungumza hapo awali wakati wa kufugua mafunzo Mkuu wa Wilaya Ndugu Joseph Mkude alisema kuwa uhakiki huo hauna budi kuleta takwimu sahihi zitakazoepusha wanufaika hewa kama ilivyokuwa imetokea pale awali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndg.Haji Mnasi alisema kuwa watalaam watakaokwamisha zoezi hawatavumiliwa na hatua za kiutumishi zitachukuliwa dhidi zao.
Kwa siku ya kwanza vijiji vya Tarafa ya Bulambya ndivyo viliweza kuhakikiwa huku siku ya pili ikihusisha vijiji vingi vya Bundali.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unatekeleza Mpango Kunusuru Kaya Maskini kwa lengo la kuwezesha Kaya Maskini kuongeza kipato,fursa na uwezo wa kugharimia mahitaji muhimu ukiwa unatekelezwa katika Mitaa na Vijiji vyote vya Tanzania Bara na Shehia zote za Unguja na Pemba kwa Zanzibar.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa