Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi, ametoa rai kwa watumishi wa Umma kuzingatia Maadili, Uwazi na Uwajibikaji sambamba na kuepuka vitendo vya Rushwa ili kutoa huduma bora kwa Wananchi pasipo kuwepo na upendeleo.
Akizungumza mapema leo Januari 22,2025 ambapo alifungua Semina ya Mafunzo kwa Watumishi wa Umma inayohusu kuwajengea uwezo wa kutumia mfumo wa Manunuzi wa Ki elektroniki (NeST), Mheshimiwa Mgomi amewaasa Watumishi kuzingatia ubunifu wakati wa kutoa huduma kwa wananchi ili kuweza kutekeleza kwa ufanisi fursa zilizoboreshwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha DC Mgomi amewasisistiza watumishi wa Umma kuendelea kuutumia mfumo wa Manunuzi kwa njia ipasayo ikiwemo kujua namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wakati wanapotumia mfumo huo. Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watumishi katika Mfumo wa NeST yatahitimishwa januari 23, 2025.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa