Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi, amewaongoza Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Katibu Tarafa ya Bulambya, Bi Irene Lymo , pamoja na Wataalamu na Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ileje , kutembelea na kukagua utekelezwaji wa Miradi ya Afya na Elimu katika Wilaya ya Ileje.
Ziara hiyo imefanyika mapema leo Februari 27, 2025 ambapo Mkuu wa wilaya amewapongeza wasimamizi wa Miradi hiyo kwa kuzingatia Ubora, Ufanisi na Weledi ili kufanikisha miradi hiyo itakayoleta tija na ustawi kwa wananchi katika Wilaya hii.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa siku ya leo ni pamoja na ujenzi wa Vyumba viwili vya Maabara Shule ya Sekondari Ibaba unaogharimu kiasi cha shilingi Million 34.9 ambapo Fedha kutoka Serikali Kuu ni Shilingi Milion 30, Fedha kutoka Halmashauri zikiwa ni shilingi Milion 4,960, 800 pamoja na Nguvu ya wananchi ambapo mpaka sasa umefikia hatua ya ukamilishaji.
Ujenzi wa kituo cha afya Ndola unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 500,000,000/= Kutoka Serikali kuu , huku Halmashauri ikichangia kiasi cha Milion 85,000,000/= pamoja na Nguvu za Wananchi ili kukamilisha mradi huo zikiwa ni Shiling Laki Sita (600,000/=).
Aidha mheshimiwa Mgomi ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Vyumba viwili vya Maabara Shule ya Sekondari Ndola unaogharimu kiasi cha shilingi Milion 34.9 ambapo Fedha kutoka Serikali Kuu ni shilingi Milion 30, fedha kutoka Halmashauri zikiwa ni shilingi Milion 4,960, 800 pamoja na Nguvu ya Wanaanchi waliochangia shilingi Milion 5,160,000/=
Miradi iliyotembelewa na Kukaguliwa siku ya leo inatarajiwa kuleta ahueni kwa Wananchi hii ikiwa ni pamoja Uboreshaji wa Huduma za Afya kwa kwa Mama na Mtoto pamoja na kuondoa umbali kwa w\Wananchi kupata huduma za afya, aidha Miradi ya Elimu itasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi na kuwa hazina kwa Taifa la Tanzania .
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa Fedha zinazokamilisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hii, aidha amewahimiza wasimamizi wa miradi hiyo kuikamilisha kwa wakati ili ianze kutoa huduma kwa wananchi katika Wilaya ya Ileje.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa