Alitoa kauli hiyo wakati kikao cha siku moja kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya alipokuwa akizungumza na baadhi ya mashirika hayo ikiwa ni pamoja na kufahamiana pamoja na kutoa taarifa za shughuli zao.
Alisema kuwa mashirika hayo yapo kwa mujibu wa sheria,hivyo ngazi zote za uongozi kuanzia watendaji wa vijiji hadi wilaya hawana budi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vile mchango wao kwa serikali ni mkubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Pamoja na mambo mengine Mhe.Mgomi alishukuru wadau hao kwa kuwa na ushirikiano mkubwa na serikali yao katika Nyanja mbalimbali pamoja na matukio mengine.
Aliongeza kuwa kufanya hivyo wanachangia kupunguza mzigo serikali katika kuwahudumia wananchi wake,matokeo ya kazi zao katika wilaya ya Ileje yanaonekana hivyo akatoa wito kwa wadau hao kutoa taarifa juu ya yeyote anayewakawamisha
Hata hivyo,hakusita kuyaelekeza mashirika hayo kujikita kwenye majukumu yaliyopitishwa wakati wa kusajiliwa na kujiepusha kuwa wakala wa mambo yanayoweza kudhalilisha taswira mila na desturi zetu.
Kwa upande wao wadau hao waliishukuru serikali kwa mwaliko huo pamoja na ushirikiano wanaoupata toka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya.
IRDO na HRNS ni baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho ambacho kilikuwa na mjadala wa kimaboresho kiutendaji hususani kwenye shughuli zinazoweza kuingiliana.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa