Prof.Ndalichako azindua Chuo cha VETA Ileje huku wahitmu wa Vyuo Vikuu nchini wakitakiwa kuchangamkia fursa za masomo katika vyuo vya Ufundi Stadi hali itakayowasaidia kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini.
Hayo yalisemwa na viongozi wakati wa ufunguzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Ileje mkoani Songwe kinachotarajiwa kuwa mkombozi kwa vijana wa Wilaya hiyo pamoja na mkoa mzima wa Songwe.
Akizungumza na wananchi chuoni hapo pamoja hotuba yake kurushwa mubashara na Kituo Cha Redio cha Ileje Fm 105.3 Prof.Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi alisema kuwa Vyuo vya ufundi Stadi vimekuwa msaada kwa serikali kufikia malengo yake ya Tanzania ya Viwanda kupitia watalaam wanaozalishwa vyuoni humo.
Aliongeza kuwa kwa kutambua mchango huo serikali imewekeza mabilioni ya fedha katika ujenzi wa vyuo pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia huku akitaja ujenzi unaondelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama vile Nkasi,Muleba,Babati,Kasulu na maeneo mengine ili kuweza kuzifikia wilaya zote.
Palaslas Bujuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA hapa nchini akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa udahili kwajajili ya wananchuo hao si wa kibaguzi kwakuwa unachukua watu wote kuanzia Darasa la Saba hadi Chuo Kikuu akitoa wito kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu kutumia fursa hiyo badala ya kusubiri kuajilriwa hali aliyosema imekuwa ikichelewesha maendeleo yao.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela aliwaomba wakazi wa Mkoa wa Songwe kuunga juhudi za Mhe.Rais katika mipango yake ya kuisogeza mbele Tanzania kimaendeleo pamoja na jinsi alivyojenga ushirikiano katika jamii pamoja na nidhamu nzuri katika matumizi ya pesa zinazokusanywa.
Aidha kiongozi huyo alishukuru viongozi wa Wilaya Ileje kwa kuibua wazo hilo na kupongeza serikali ya Japani kwa mchango wao wa milioni 154 zilizoweza kuchangia ujenzi wa majengo mawili ya awali ambayo yameweza kukamilishwa na VETA.
Tafrija hiyo ilihusisha makundi mbalimbali ya wadau wa maendeleo ya wilaya wakiwemo viongozi wa serikali,dini,mila pamoja na wakazi wa vijiji vya Itumba na Isongole.
Chuo cha Ufundi cha Ileje kinakuwa ni chuo pekee cha VETA ndani ya mkoa wa Songwewenye zaidi w\ya wakazi milioni 1.2 na viongozi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakiomba serikali kukipitisha kuwa chuo cha mkoa.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa