Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ileje Bi.Bless Mwakyusa ambae pia ni Afisa Utumishi wa Wilaya hii, amekabidhi msaada wa vyakula na mahitaji kwa Kaya 44 za wananchi wa Kata ya Mbebe ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Wilaya hii.
Msaada huo umeakabidhiwa mapema leo Disemba 2,2024, katika ofisi ya kata hiyo ambapo Bi Bless amewasisitiza wananchi wa Kata hiyo kuendelea kuchukua tadhahari katika kipindi hiki cha mvua sambamba kuwa watulivu kwani Serikali ni Sikivu na ipo tayari kutoa msaada muda wowote panapotokea majanga kwa wananchi wake.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ametoa rai kwa watendaji wa Vijiji kuhakikisha msaada huo unawafikiwa walengwa ambao nyumba zao ziliharibika kutokana mvua iliyoambatana na upepo. Msaada uliokabidhiwa kwa walengwa ni pamoja na Mahindi debe 88, Maharage kilo 60, pamoja na Sukari kilo 88.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa