Hayo yalisemwa na wadau mbalimbali wakati wa madhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika kimkoa katika Ukumbi wa Radwelo Itumba Wilayani Ileje
Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.John Palingo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi aliwataka wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa (Songwe Press Club)
Palingo alisema kuwa waandishi wa habari hawana budi kwenda kwa wananchi na kuandika habari za uchunguzi ambazo mara nyingi huwa mkombozi wa jamii na msaada kwa serikali kwa vile huja na taarifa mpya zenye kusisimua.
Mohamed Mwala Diwani wa Kata ya Itumba na Mwandishi wa Habari mstaafu alisema kuwa waandishi wa habari hawana budi kwenda kwa wananchi wa vijijini kuibua habari badala ya kusubiri ziara za viongozi zinazoambatana na malipo hali aliyosema inamnyima mwandishi uhuru wa kueleza ukweli.
Kayolo Msongole Katibu wa MUJATA wilayani humo aliwataka wanahabari hao kujiepusha kuandika habari za uongo akisema kuwa hushusha hadhi ya taaluma,hata kama ni mwanahabari mmoja akiwa na tabia hiyo huweza kuchafua wengine wote na kupoteza uaminifu katika jamii.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo yalilenga kuwapa fursa wadau wa habari pamoja na wananchi kutoa maoni yao juu ya utendaji wa vyombo vya habari katika mkoa wa Songwe.
Awali Mwenyekiti wa Klabu hiyo mkoani humo Ndg.Stephano Simbeye alimweleza Mgeni Rasmi kuwa waandishi wa mkoa huo wanapenda sana kuwafikia wakazi wa vijijini lakini wanakwama badala yake kusubiri misafara ya viongozi kutokana na uchanga wa Klabu ambayo ilianzishwamiaka michache iliyopita.
Kauli Mbiu ya mwaka huu katika Madhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ni “Habari kwa Manufaa ya Umma’’
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa