Katika kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19 Wilaya ya Ileje mkoani Songwe imepokea vifaa kwaajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Vifaa hivyo,vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 13 vilitolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la One Accre Fund linalojihusisha na masuala ya kilimo hapa nchini kwa baadhi ya wilaya,Ileje ikiwa mojawapo
Akizungumza kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Kiongozi wa Mradi kwa mikoa ya Songwe na Mbeya Ndg.Hussein Majabali alibainisha vifaa hivyo kuwa ni sabuni, groves vitagawiwa kwa wakulima 3243 katika vijiji 19 vinavyohudumiwa na mradi huo kwa wilaya ya Ileje.
Hussein aliongezeza kuwa zaidi ya vipeperushi 920,000 vitagawiwa kwa wananchi bila kujali iwapo wanahudumiwa na mradi huo.
Kiongozi huyo,alisema kuwa msaada unalenga kulinda afya za wakulima ambao ni wadau wakubwa mradi huo.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo Ofisini kwake Mkuu wa Wilaya hiyo alishukuru kwa msaada huo huku akiomba wadau wengine kujitokeza ili kuzendelea kukamilisha mahitaji ya vifaa hivyo akisema jumla ya shilingi milioni 174 zinahitajika.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa hadi sasa jumla ya shilingi Milioni Mbili zimekusanywa toka kwa wadau mbalimbali kwaajili ya zoezi hilo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa