18/03/2022 Na,Daniel Mwambene Ileje maadhimisho
Hayo yamejili Ijumaa 18,Machi,2022 wakati Wilaya hiyo ikiadhimisha Mwaka mmoja wa uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassan baada yaa kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli.
Akikabidhi sehemu ya mikopo hiyo ambazo ni pikipiki 10 na bajaji 2 pamoja na mfano wa hundi ya thamani ya pesa hiyo Mkuu wa Wilaya Mhe.Anna Gidarya alilitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kuwaongezea elimu ya Usalama wa Barabarani vijana hao ili kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikiwaandama bodaboda mara kwa mara.
Mhe.Gidarya aliongeza kuwa mikopo hiyo imewafikia walengwa kwa sababu ya mfumo mzuri wa uongozi wa Mhe.Samia Suluhu Hasaan Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akisoma taarifa ya Wilaya ya Ileje kweny viwanja vya Stendi ya IItumba Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndg.Matias Mizengo alisema kuwa kiasi cha Tzsh.6,316,446,139.55 zimepokelewa kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Machi 2022 kwaajili ya kutekeleza Miradi ya sekta ya Elimu Msingi na Sekondari pamoja na Afya.
Awali Afisa Maendeleo ya Jamii wa wialaya hiyo Ndg.Rodrick Sengela akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika kuwawezesha vijana,wanawake na watu wenye ulemavu alisema kuwa jumla ya vikundi vya vijana 11 na watu wenye ulemavu wawili vimekopeshwa kiasi hicho cha pesa kwa kipindi cha 2021/2022.
Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake waliopata mikopo ya pikipiki Daud Mwanja aliishukuru serikali kwa jinsi inavyotoa elimu ya mikopo kupitia Idara ya maendeleo ya Jamii.
Kabla ya kuelekea kwenye viwanja hivyo vya maadhimisho Mkuu wa Wilaya aliongoza viongozi wa wilaya hiyo na wakazi wa Kijiji cha Isongole ujenzi wa shule mpya ya Msingi katika Kitongoji cha Ipapa ambayo imekumbwa na ubovu wa barabara inayofika kwenye mradi huo baada ya kupokea Tzsh.Milioni 400.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa