UNESCO watembelea Mradi wa Radio Ileje
Na: Daniel Mwambene, Ileje
Kwa muda wa siku mbili wilaya ya Ileje mkoani Songwe ilikuwa na ugeni toka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO).
Ziara hiyo iliyohusisha watafiti wawili Bw.Boncani Nassor toka Tanzania na Bi.Chashe Heallesby toka London Uingereza ililenga redio redio ya kijamii ya Ileje Fm inayosikia kwenye mitabendi 105.3.
Wageni hao waliweza kuonana na Wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao pamoja na Mkurugenzi Mtendaji huku Kikundi Cha Ileje Mashariki (BWELUI) ambacho ni mdau mkubwa wa redio hiyo kikiwakilishwa na Mkurugenzi wake Mzee Lucas Mtafya.
Katika kikao hicho waliweza kupata maelezo jinsi halmashauri inavyoshiki katika kukiendesha,kukitumia kituo hicho cha redio katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Pamoja na mambo mengine pia wageni hao waliweza kuupokea changamoto kadha zinazokabiri redio hiyo ambayo kwa sasa haipo hewani kutokana na kukosa umeme kwenye minara baada ya majenereta yaliyokuwa yakitumika kuharibika karibu miezi miwili iliyopita.
Pia ziara hiyo iliweza kuwakutanisha wageni hao na watangazaji,wasikilizaji na wadau wengine wa redio ili kuweza kukamilisha safari yao ya kitafiti.
Ikiwa hewani kwa takribani mwaka mmoja na nusu redio hii ni kati ya redio mbili tu zinazorusha matangazo yake katika mkoa huu mpya wa Songwe ikiwemo Ilasi fm inayorusha matangazo yake toka Vwawa ambayo ni Makuu ya Mkoa wa Songwe na hakuna kituo chochote cha kurushia matangazo ya televisheni.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa