Wanawake, Vijana na Walemavu katika kujibu changamoto ya ukosefu wa mitaji, hususani wanawake Wajasiriamali.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe.Omary Mgumba, wakati akijibu kilio cha ukosefu wa mitaji na changamoto za mikopo ya wajasiriamali inayotolewa na Halmashauri nchini kwenye maadhimisho ya sherehe ya Siku ya Wanawake duniani ambazo zilifanyika kimkoa Ileje.
Mgumba alisema kuwa katika makisio ya Bajeti ya mwaka huu 2022/23 Mkoa huo unatarajia kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya Mikopo, ambapo jumla ya shilingi milioni 600 zitatolewa kwa wanawake.
Mgumba alisema amewaelekeza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa huos kuacha kutoa mikopo ya kugawana umasikini bali waweke utaratibu mzuri wa kutoa mikopo kwa watu wachache, ili isaidie kutatua changamoto ya mitaji midogo.
Awali akisoma risala katika maadhisho hayo, Ofisa maendeleo ya Jamii Mkoa wa Songwe, Atusungukye Dzombe, amesema pamoja na jitihada za kutekeleza dhana ya usawa bado kundi la wanawake limeendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa