Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bi. Nuru Waziri Kindamba amesema Wilaya ya Ileje na Mkoa kwa ujumla unapambana kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni ambalo kwa muda mrefu lipo mkoani Songwe linapungua kama siyo kumalizika kabisa.
Mkurugenzi Kindamba ameyasema hayo leo Machi 19, 2024 wakati akiongea na ugeni kutoka Shirika la UNICEF pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Canada nchini Tanzania ambao kwa pamoja wanafadhili miradi mbalimbali ndani ya wilaya hii. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bi. Nuru Waziri Kindamba amesema Wilaya ya Ileje na Mkoa kwa ujumla unapambana kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni ambalo kwa muda mrefu lipo mkoani Songwe linapungua kama siyo kumalizika kabisa.
Mkurugenzi Kindamba ameyasema hayo leo Machi 19, 2024 wakati akiongea na ugeni kutoka Shirika la UNICEF pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Canada nchini Tanzania ambao kwa pamoja wanafadhili miradi mbalimbali ndani ya wilaya hii.
Miongoni mwa mradi mkubwa ni GREAT ambao unalenga kuwezesha uelewa kwa vijana juu ya uzazi wa mpango pamoja na afya ya uzazi lakini sambamba na hilo ni kuwezesha jamii kupata elimu stahiki juu ya mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
“Tatizo la mimba za utotoni ambalo Songwe inalo tunaanza kupunguza sasa kwasababu vijana wajue sasa jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi lakini pia kutumia ngono salama ili kujikinga sasa na pia upatikanaji wa mimba za utotoni lakini pia kuondokana na hiyo tabia.” Amesema Mkurugenzi Kindamba.
Aidha katika hatua nyingine Mkurugenzi Kindamba amesema katika suala zima la kuwaongezea vijana uwezo tayari kuna namba kubwa ya vijana ambao wameshapewa mafunzo na wapo tayari kutoa mafunzo hayo kwa vijana wengine hii ikiwa ni hatua muhimu ya kuhakikisha kunakuwa na mwendelezo wa kuhakikisha elimu hii inafikia kundi kubwa la watu hususan vijana.
Akiwasilisha ripoti mbele ya wahisani, Josepha Mgimba ambaye ni Muuguzi katika Hospitali ya Mbebe wilayani hapa amesema tayari vijana 96 ambao hawajazaa wamefanikiwa kutumia njia ya uzazi wa mpango ambao miongoni mwao wanawake 46 na wanaume 50.

Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa