Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Omary Mgumbaamemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuhakikisha TAKUKURU inafanya uchunguzikwa Miradi yote ya Maendeleo ya Wilaya ya Ileje ili kubaini ubadhirifu wafedha.
Mgumba alitoa maagizo hayo wakati wa ukaguzi wa Miradi ya Maendeleouliofanywa na Kamati ya Siasa ya Mkoa ikiongozwa na Komredi Elyniko Mkolakatika miradi ya elimu na afya.
“Itaundwa kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa Miradi ya Maendeleo Wilayaya Ileje kuchunguza kwa miaka mitatu ili kubaini ubadhirifu huo”.AlisemaMhe.Mgumba.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi na kwenye kikao cha majumuishokatika Ukumbi wa VIM Mwenyekiti wa CCM Komredi Mkola alisema kuwa viongozi waChama cha Mapinduzi wanatakiwa kuwa macho ya chama na serikali katikakuhakikisha kuwa pesa za miradi ya maendeleo zinatumika vema.
“Miradi ya Maendeleo ndiyo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na huwa nimkataba kati ya serikali na wananchi ambao ni wapiga kura”.AlisisitizaMwenyekiti huyo.
Baadhi ya miradi iliyomkera kiongozi huyo na kushindwa kuficha hisia zakeni ujenzi wa Zahanati ya Chembe zilikopelekwa milioni 50 huku jengo likiwalilishajengwa na wananchi kwa nguvu zao kwa muda mrefu.
Maeneo mengine ni ujenzi wa vyoo Shule Msingi Mpakani na katika Sekondariya Ikinga pamoja na ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Kafule ambakotaarifa za viongozi wa maeneo hayo zilikuwa zikitofautiana.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilayanihumo ilikataa baadhi ya Miradi ya Maendeleo hali iliyopelekea Mkuu wa Wilayahiyo Mhe.Anna Gidarya kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi waliohusika katikaujenzi huo ili kupisha uchunguzi.
Hata hivyo Kamati hiyo iliweza kupongeza hatua za ujenzi na ubora wamajengo katika wodi tatu kwenye Hospitali ya Wilaya ambako serikaliilishapeleka milioni 500.s