Pongezi hizo zimetolewa mapema leo Jumatatu Septemba14,2020 kwa nyakati mbili tofauti na Naibu Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Mhe.Omary Mgumba wakati wa ziara ya siku moja ya kuangalia msimu mpya wa ununuzi wa mahindi kwenye soko la Isongole.
Akizungumza kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya Waziri huyo amesema kuwa aina ya karanga zinazozalishwa wilayani humo imekuwa maarufu sana hapa nchini na kwa nchi jirani kiasi cha kuvunja soko la karanga za aina nyingine huku likiitangaza vema wilaya ya Ileje na Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kwenye soko la Isongole waziri Mgumba amesema serikali ipo tayari kuunga juhudi hizo za wakulima kwa kuwatengenezea mipango itakayowawezesha kuzalisha zaidi ili kuondokana na umaskini.
Ameitaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya barabara ikiwemo ya Mpemba Isongole inayojengwa kwa kiwango cha lami ,ujenzi wa masoko,maghala pamoja na vihenge vya kuhifadhia mazao hayo.
Joseph Nyembele mmoja wa wakulima wa Isongole ameiomba serikali kuharakisha kununua mazao ya wakulima kila msimu wa mavuno unapomalizika ili kuwawezesha wakulima hao kufanya shughuli zao za maendeleo zikiwemo ada za shule na vyuo kwa watoto.
Taarifa ya kilimo ya wilaya hiyo iliyosomwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Ndugu Haji Mnasi ilieleza kuwa wilaya hiyo ina jumla ya hekta 190,800 huku eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 101,600 ambapo kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020 hekta 72,223 ziliweza kulimwa na kupata jumla ya tani 348,211.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa