Wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo ya siku moja wilayani hapa Januari,18,mwaka huu baadhi ya wakufunzi na wanachuo wameeleza kufurahishwa na hali hiyo hususani kwenye Mradi wa Shamba la Miti la Iyondo-Mswima.
Mkuu wa Msafara Mkufunzi Mwandamizi Balozi Noel Kaganda amempongeza Mkuu wa Wilaya pamoja na uongozi mzima wa wilaya na wananchi kwa kushikamana katika kutunza mazingira.
Meja Jenerali Wilbert Ibuge mmoja wa wakufunzi hao akielezea umuhimu wa mradi huo ameshauri uongozi wa shamba hilo kuhakikisha unashirikiana na wananchi wanaozunguka shamba hilo ili kuwatengenezea fursa zinazoweza kuwepo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ileje Anna Gidarya amewaeleza watalaam hao kuwa tayari wakazi waliokuwepo katika makazi ya soko la Katengele ndani ya mradi wameshahama baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika hivyo kuongeza usalama zaidi wa mradi.
Awali Jovan Emmanuel Mhifadhi wa shamba hilo alisema kuwa licha ya kujihusisha na upandaji miti pia wamekuwa wakigawa miche ya miti kwa vijiji vinavyozunguka mradi.
Wanachuo hao ni kutoka Tanzania pamoja na mataifa mengine yakiwemo Kenya,Uganda,Misri na Afrika Kusini.
Shamba la Iyondo-Mswima lipo kwenye vilele vya milima yenye misitu ya asili na kupandwa ambayo ni chanzo cha mito mingi ikiwemo Mto Songwe na Kiwira inayomwaga maji katika Ziwa Nyasa.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa