Mwenge wa Uhuru watua nyumbani kwa Cheyo
Mwenge wa Uhuru watua nyumbani kwa Mzee Cheyo utunzaji mazingira wampaisha asema ni njia mojawapo ya kumuenzi kwa vitendo Baba wa Taifa hayati Mwl.J.Nyerere.
Hatimaye Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Siku ya tatu mkoani Songwe tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan umeweza kufika nyumbani kwa Mzee Gidion Cheyo mbunge mstaafu wa Ileje na liyewakuwa Waziri Mwandamizi Awamu yaTatu.
Akikagua uhifadhi wa msitu unafanywa na mzee huyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu Ndugu Mzee Mkongea Ali alipongeza juhudi hizo akisema ili kulinda vyanzo vya maji kama ulivyo ujumbe wa mwenge mwaka huu jamii haina budi kuunga juhudi za watu kama hao.
Msitu wa hifadhi wa mzee cheyo una ukubwa wa zaidi ya ekari 28 ukisheheni miti mingi ya asili ambayo anasema alishapata hati ya umiliki wa msitu huo tangu 2001.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo alisema kuwa wamekuwa wakinufaika na msitu huo kwa kupata hewa safi pamoja dawa.
Wilaya ya Ileje iliupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa ndugu zao wa Songwe ili nao baada ya kumaliza mbio zke utakabidhiwa kwa Wilaya ya Momba
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa