Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Wilayani Ileje hapo siku ya Ijumaa katika Kitongoji cha Ileya Kijiji cha Ndola Kata ya Ndola.
Kisha utakimbizwa huku,ukiweka mawe ya msingi,kuzindua pamoja na kukagua Miradi ya Maendeleo na mkesha utakuwa katika Stendi ya Isongole Kijiji cha Isongole.
Hapo tarehe 17/09/2022 Asubuhi ya Jumamosi Mwenge utakabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika Kijiji cha Nandanga.
Akizungumza katika vikao mbalimbali vya maandalizi Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Anna Gidarya amewataka wananchi wote kushikamana ili kufanikisha mbio hizo kwa mwaka huu 2022.
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 ni : Shiriki Kikamilifu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Maendeleo Endelevu ya Tanzania
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa