Taarifa zilieleza kuwa mnyama huyo alianza kuonekana katika Kijiji cha Izuba,akielekea Itumba vitongoji cha Chobwe,Chafwanya kisha katika Kijiji cha Isongole ambako aliuawa kwa kupigwa risasi na askari waliofika eneo la tukio.
Huku tkukio hilo likivuta umati mkubwa wa wananchi kabla hajauwawa baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo walionesha wasiwasi wao juu ya kutochukuliwa kwa tahadhari ya kutosha kwani watoto wazee na hata wanawake wakiwa wamebeba watoto mgongoni waliweza kwenda kushuhudia mnyama huyo hatari akiwa hai
Tahauki hiyo iliyoanza asuhuhi na mapema iliweza kufika hatima yake majira ya saa nane mchana baada ya kumpiga risasi na kisha kuondolewa eneo hilo huku kila mmoja akitaka kupata sehemu ya nyama hiyo.
Kamera yetu iliweza kushuhudia hadi hatua ya uchunaji ngozi na upasuaji ambapo ilielezwa na wasimamizi wa zoezi hilo kuwa nyama ilitakiwa kugawiwa kwa makumndi mbalimbali wakiwemo machifu waliopitiwa na nyati huyo,pamoja na viongozi wengine.
Kumekuwa na taarifa tofauti za alikokuwa ametokeamnyama huyo huku wengi wakisema ametokea Mbuga za Nyika Malawi ambako mara kadha kumekuwa na utoro wa wanyama hao wakiwemo simba ambao huvuka mpaka kuingia hapa nchini.
Hata hivyo wengine wanadai kuwa mnyama huyo atakuwa alitokea kwenye mapori makubwa yaliyopo Zambia katika Wilaya ya Mbala.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa