Akizungumza katika maeneo ya miradi Dkt.Michael alipongeza juhudi zinazofanywa na wananchi katika kutoa nguvu zao kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile afya na elimu akiongeza kuwa mchango wao huo lazima utambuliwe na kuthaminishwa.
Aliongeza kuwa,miradi ya maendeleo ikitekelezwa ovyo lawama zote zinaelekezwa kwa serikali,hivyo ni jukumu la kila mtumishi wa serikali kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake ili kujenga taswira nzuri ya serikali kwa wananchi wake.
Pamoja na mambo mengine kiongozi huyo alisistiza watumishi kujiamini kwenye nafasi zao za uongozi huku wakijua kuwa kufanikiwa kwao katika ngazi moja kunaweza kuwapeleka katika ngazi nyingine kubwa zaidi ya uongozi.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhe.Happiness Seneda alieleza kufurahishwa kwake na utekelezaji wa maagizo kwenye baadhi ya miradi hususani katika hospitali ya wilaya kwenye jengo la mionzi akisema hatua iliyofikiwa ni nzuri na inaashiria kuanza karibuni kwa utoaji wa huduma ya X - Ray ambalo ni tatizo kubwa la kimkoa.
Aidha Mhe.Seneda alipongeza uongozi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Ileje iliyopo Kata ya Chitete kwa jinsi wanavyowalea wanafunzi kuwa wasafi katika mabweni yao akisisitiza waendelee pia kuwalea katika maadili ya Kitanzania.
Ziara hiyo ya siku moja ilikuwa na makundi mawili ya viongozi wa mkoa na wilaya,moja likiongozwa na Mkuu wa mkoa na jingine likiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa na kuwezesha kukagua miradi hiyo 12 yenye thamani ya Tzsh.8,983,353,229.21/=.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuona hali halisi,ubora wa miradi,muda wa utekelezaji uliopangwa,taratibu za manunuzi,changamoto,ushirikishwaji wa wananchi katika miradi ya maendeleo pamoja utekelezaji wa maagizo8, ya miradi husika.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa